IPAMBE RAMADHAN YAKO KWA SMS,STATUS HIZI

IPAMBE RAMADHAN YAKO KWA SMS,STATUS HIZI

Sunday, May 5, 2019, May 05, 2019
بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمنِ الرَّحِيم
WAKATI WAISLAMU WAKIINGIA KATIKA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI 2019 NASI TUNGEPENDA KUUNGANA KWA KUKULETEA JUMBE ZA MANENO KULINGANA NA WAKATI HUU WA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI.JUMBE HIZI YAFAA KUSHARE NA NDUGU JAMAA NA MARAFIKI NA KWALO FAIDA KUBWA ITAPATIKANA.TUNAWATAKIA WAISLAMU WOTE KHERI YA RAMADHANI..
  1. Funguo ya mafanikio inapatikana katika Qur'an. Tunaweza kupata baraka na uongozi kama tunavyoisoma pamoja katika siku za Ramadan. Furaha ya Ramadani!
  2. Na Mwenyezi Mungu akuletee baraka nyingi Ramadan hii, Ramadan yabaraka kwako na familia yako.
  3. Katika mwezi wa Ramadan, ninakutakia wiki 4 za baraka, siku 30 za usafi wa roho, na masaa 720 ya mwangaza. Furaha ya Ramadani!
  4. Image result for ramadan quotes
  5. Kama mwezi wa Ramadan unapoanza, kauliana kwa heshima, uwatendee wengine kwa huruma, tembea kwa upole na usali kwa dhati. Mwenyezi Mungu akubariki wewe na familia yako.Ramadan yabaka.. !!
  6. Mwenyezi Mungu akupe amani, utulivu, uvumilivu na afya katika mwezi huu wa "RAMADAN" pamoja na baraka zake .Ramadan Ya kheri kwako.. !!
  7. Mwezi mtakatifu wa Ramadan unakuja sasa,Allah achukue ibada zetu na kusamehe makosa yetu yote.Ramadhani Mubarak kwako na familia yako.
  8. Image result for ramadan quotes
  9. Mwezi mtukufu wa Ramadhani Mwenyezi Mungu Anatuwezesha Kufanya zaidi na zaidi yale yaliyo mazuri ili kutuongezea dhawabu na kuepushwa na moto... Na Mwenyezi Mungu atasamehe dhambi zetu.
  10. Mapenzi ya Allah yawe maliwazo kwako, Akuruzuku imani na huba moyoni mwako, Pepo yake Rahmani iwe ndio makaazi yako, Akupe yalo mema kuzidi fikra zako. ***AMEEN***.Ramadhani ya baraka kwako
  11. Mwezi mtukufu umewadia, Yarraby tunusuru na Balaa za Duniya, Tufaulu Mitihani ya kilimwengu, Tuwe ni wenye kukumbuka na kushukuru Fadhla na Ukarimu wako. ****AMEEN!!!**** Ramadhani Mubarak!!!
  12. Image result for ramadan quotes
  13. Rabbi tuvike libasi Leo na kesho Qiyama Tuondoshe wasi wasi Utwepushe zahma Tusitiri na maa'si Tusiwe wenye kuzama Awe mbali nasi Ibilisi Nasi peponi yawemakazi yetu, Amiyn **Ramadhani Kareem**
  14. Nuru ya allah imulike kwako,ikutimizie mahitaji yako.riziki ya halali iwe pato lako,upendo uwe chakula chako,nyayo yako kuu iwe qur'an.Ramadhani karim
  15. Yuko wapi kama Wewe Mja ulo na Imani, Dua zitakabaliwe uombazo kwa Manani, Milango Ufunguliwe na Malaika Peponi, Haja utimiziwe ulonuia Moyoni,iliyoje thamani,kuifika ramadhani.
  16. Image result for ramadan quotes
  17. Amesema mtume wa Allah (s.a.w): ''ramadhani mpaka ramadhani,ijumaa mpaka ijumaa,swala mpaka swala ni vifutio vya madhambi zikiepukwa dhambi kubwa kubwa" tumuombe Allah kwa huruma zake Ramadhani hii inshallah atufutie madhambi yetu tuliyofanya tukiwa tunajua au hatujui. 
  18. In His infinite mercy, Allah has
    sent the light of Ramadan to erase the night. He has sent the month of the Qur’an so that He might
    elevate us and bring us from our isolation to His nearness
  19. Ramadan Reminder
  20. Bismillahi naanza, kwa jina lake Rabuka,
    Subhanau wa kwanza, Maliki si mshirika,
    Peke yake ni muweza Karima mwenye baraka,
    Ramadhani imefika, tuyatende yalo mema!

    Wa Rehema Rahmani, tuombe atujalie,
    Mafisadi wa zamani, mbali tuwafukuzie,
    Na wanaokuja wageni, nchi tuwakatalie,
    Ramadhani imefika, tuyatende yalo mema!

    Kama wewe ni fisadi, mfungo uwe nafasi,
    Uuache ukaidi, na dini usiiasi,
    Uzilipe zote kodi, sikaribishe mikosi,
    Ramadhani imefika, tuyatende yalo mema!

    Al watani natama, wakijiji ninakoma,
    Na mwezi ukiandama, wa mfungo wa lazima,
    Nawatakieni mema, mfungao bila hima,
    Ramadhani imefika, tuyatende yalo mema

TerPopuler